KIKOSI cha Azam FC kimetinga hatua ya 16 bora kibabe baada ya jana kuwanyoosha kwa mabao 2-0 Pamba FC mchezo uliochezwa Uwanja wa Chamazi.
Azam katika hatua ya tatu waliwanyoosha Madini FC kwa mabao 2-0 na kutinga hatua ya raundi ya nne ambapo wamefanikiwa kupita kibabe.
Mabao yote ya Azam FC jana yalifungwa na Ranadhani Singano 'Messi' kipindi cha kwanza dakika ya 18 na kipindi cha pili dakika ya 52.
Mchezo wao unaofuata utakuwa dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora utakaochezwa kati ya Februari 22 au 25 mwaka huu Uwanja wa Chamazi.
0 Comments