Uwanja wa klabu ya Simba unaojengwa huko Simba umebakisha kidogo kufikia hatua ya kuwekewa nyasi bandia kwa ajili ya timu kuanza mazoezi.
Kwa mujibu wa mmoja kati ya mafundi katika uwanja huo, Aloyce Joseph, amesema tayari mabomba ya kupitisha maji chini yameshawekwa.
Ameeleza pia, zoezi litakalofuata na kuwekwa kwa nyasi bandia ambazo zitatandazwa chini na baada ya hapo kutawekwa fensi kuzunguka uwanja.
"Mpaka sasa tumeshakamilisha uwekwaji wa mabomba chini na kitakachofuata ni kutandaza nyasi bandia na kisha zoezi la fensi litafuata na timu itakuwa tayari kuanza mazoezi" alisema.
Mpaka sasa Simba imekuwa ikitumia uwanja wa Bocco Veterani kufanyia mazoezi yake katika mechi za ligi na kimataifa kitu ambacho huwafanya watumie gharama kubwa za kulipia.
0 Comments