Windows

KISA YANGA, SIMBA YAPEWA ONYO KALI


Mchezaji wa zamani wa Yanga, Bakali Malima 'Jembe Ulaya, amewatahadharisha Simba kuwa mechi ya watani wa jadi haitabiriki.

Jembe Ulaya amefunguka kutokana na Simba kuichukulia Yanga ya kawaida kwa kipindi hiki huku akiwaonya kuwa wakija na dharau wanaweza kupoteza mchezo huo.

Mchezaji huyo aliyetamba miaka ya nyuma, ameeleza kuwa mechi inayokutanisha Simba na Yanga huwa haitabiriki kirahisi na badala yake yoyote aliyejipanga vema atapata matokeo.

Kuelekea mechi hiyo ya watani wa jadi Malima amesema timu zote mbili zinapaswa kujipanga vema ili kuhakikisha zinacheza kusaka alama tatu.

"Mechi hizi huwa hazina utabiri, unaweza ukaiona Yanga mbovu kwa sasa lakini ikaja ikafanya maajabu zaidi kwa Simba, hivyo timu iliyojipanga vilivyo ndiyo itapata matokeo kwa kutegemeana na namna ambavyo mbinu zitatumika uwanjani" amesema.

Post a Comment

0 Comments