Kocha mkuu wa Klabu ya Yanga Mwinyi Zahera ametoa neno kwa Uongozi wa klabu ya Simba hasa kwa Kocha na benchi la Ufundi kuelekea mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa barani Africa dhidi ya klabu ya National Alahly ya nchini Egypt. Mechi inayo tarajiwa kupigwa Jumamosi wiki hii.
Akiongea kupitia Azam TV Kocha huyo alisema,"Kocha wa Simba na benchi lake wanapaswa kuwaandaa wachezaji kiakili (mentality) kueleka mchezo huo wa hapo Jumamosi.
"Vinginevyo wachezaji wataingia uwanjani wakiwa na maumivu ya kufungwa kwenye mchezo uliopita ambao walipoteza dhidi ya As Vita ya Congo kwa 5-0. Hivyo suala la kuwatayarisha kiakili ni la muhimu sana vinginevyo wanaweza wakafungwa tena magoli matano tena" amesema.
Simba itakuwa inacheza na Al Ahly Jumamosi ya wiki hii huko Cairo wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kufungwa na AS Vita kwenye mchezo uliopita.
Kikosi cha Simba kinaondoka leo kuelekea Misri tayari kuzoea mazingira ya huko ili kutohangaika kupata tabu kabla ya mchezo kufika.
0 Comments