Zaidi ya miezi miwili sasa toka kocha mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera atangaze kuwa golikipa wake namba moja Beno Kakolanya atafute timu nyingine kwani hana nafasi tena Yanga, hiyo inatokana na golikipa huyo kugoma kwa siku kadhaa kuichezea timu hiyo akiwa anashinikiza alipwe madeni yake ya usajili.
Ilielezwa kuwa Kakolanya alikuwa anadai Yanga Tsh Milioni 15 za usajili lakini baada ya mdau wa Yanga kumpa kiasi cha pesa cha Tsh Milioni 2 alitaka kurudi aendelee kuichezea timu hiyo lakini kocha wake Mwinyi Zahera akamkataa na kusema hamuhitaji tena mchezaji huyo kutokana na kugoma.
Wote tunajua kuwa Yanga kuna kipindi ilikuwa indaiwa kama nafasi ya golikipa ilikuwa inapwaya kwa Klaus Kindoki kushindwa kumudu vyema kucheza nafasi hiyo huku Ramadhan Kabwili kutajwa kama mchezaji mdogo haamini kwa asilimia 100, AyoTV ilimpata nahodha wa Yanga Ibrahim Ajib na kumuuliza vipi kama wachezaji hawajawahi kufikiria kumuombea msamaha Beno Kakolanya kwa kocha wao Mwinyi Zahera.
“Kwenye hilo kiukwelia siwezi kuongelea chochote kwa sababu mwalimu yeye ndio mwenye maamuzi ataona kitu gani kipo sahihi kwake yeye mwenyewe ataamua, nikipewa nafasi ya kumshauri nitamshauri sababu yeye mtu mzima anaelewa namna timu ilivyo mpaka nikipewa nafasi ya kumshauri nitamshauri lakini kama sijapewa siwezi kushauri chochote”>>>Ajib
0 Comments