Mshambuliaji wa zamani wa Man United anayekipiga katika club ya Olympique Lyon ya Ufaransa Memphis Depay ameweka wazi dhamira yake ya kutaka kuihama club yake ya Lyon na kutaka kurejea England alipodumu kwa miaka 2 akiwa na Man United au mji mwingine wowote.
Depay ambaye amekuwa akiichezea Lyon toka mwaka 2017 ameeleza dhamira yake ya kufikiria kuihama timu hiyo kutokakana na kuonesha dalili za kutoupenda mji wa Lyon, hivyo alitamani kwenda kucheza mpira katika club yenye miji mizuri kama Paris, Bayern, Man City na mingine mingi.
Memphis akifanya mahojiano na jarida la alieleza hivi“Nataka kwenda katika club kama Real Madrid, Barcelona, Chelsea, Man City, PSG au Bayern nataka kwenda katika mji utakaonipendeza katika timu ambayo itataka kucheza mpira”>>> Memphis Depay
0 Comments