Windows

MTIBWA SUGAR WAPANIA KUPEPERUSHA BENDERA KIMATAIFA



BAADA ya kutinga hatua ya 16 Bora kwenye michuano ya kombe la Shirikisho, mabingwa watetezi wa kombe hilo, Mtibwa Sugar wamepania kulibeba kombe hilo tena msimu huu ili kupeperusha bendera kimataifa.

Mtibwa Sugar wamefanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kushinda hatua ya raundi ya tatu mbele ya Kiluvya United kwa ushindi wa mabao 3-0 na kuendeleza ubabe mbele ya Majimaji kwa ushindi wa mabao 2-1 michezo yote ikichwezwa Uwanja wa Manungu.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Mkuu Zuber Katwila amesema wapinzani wao walianza kwa kujiamini kutafuta ushindi ila mbinu na uzoefu wa kikosi chake uliwasaidia kupata matokeo.

"Tumepata matokeo kutokana na kujituma kwa wachezaji, tunatatambua kwamba sisi ni mabingwa watetezi hivyo ni lazima tupambane ili kubeba tena kombe letu na msimu huu, hilo linawezekana kwa kuwa tayari mwanga umeanza kuonekana.

"Ushindani ni mkubwa hilo lipo wazi, nawaandaa wachezaji wawe bora muda wote katika michuano hii ya Shirikisho pamoja na michezo ya Ligi Kuu Bara ambayo ipo mbele yetu," alisema Katwila.


Post a Comment

0 Comments