Windows

TAKUKURU yaokoa zaidi ya Sh. milioni 11



Na. Rahel Nyabali, Tabora

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU, Mkoani Tabora imeokoa zaidi ya shilingi milioni 11.4 zizokanazo na malipo hewa na ukiukwaji wa taratibu za malipo katika sekta ya afya mkoani humo.

Akizungumza na  Waandishi wa Habari,  Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Tabora Mashauri Elisante ameeleza kuwa fedha hizo zimeokolewa kutoka katika sekta ya afya baada ya kubaini kuna watumishi ambao wanajuhusisha na ubadhirifu.

Kufuatia hali hiyo, TAKUKURU Mkoa wa Tabora imejiwekea mikakati madhubuti ya kuhakikisha vitendo vya rushwa vinadhibitiwa maeneo yote yanayolalamikiwa ikiwemo kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watu wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi ili sheria ichukue mkondo wake.

 Mashauri Elisante amesema pale tunapoona pesa zinatumika sivyo tuna haki ya kurudisha imebainika kuna wafanyakazi ambao si waadalifu  kwenye idara ya afya wamefanya ubadhilifu  na tunarudisha kwa sheria kuna sekta nyingi Serikalini lakini katika afya imetambulika kuwa na ubadhilifu wa fedha za serikali.

Katika hatua nyingine, Elisante amesema TAKUKURU imejidhatiti kikamilifu kufuatilia miradi ya maendeleo katika idara za afya, maji na ujenzi hatua ambayo inalenga kudhibiti mianya ya rushwa  jambo ambalo litasaidia miradi ya selikari kukamilika kwa wakati.

Aidha TAKUKURU  Mkoa wa Tabora imeshinda kesi sita kati ya kesi saba zilizofunguliwa mahakamani zikihusisha vitendo vya rushwa kwa kipindi cha mwezi Oktoba 2018 na Disemba 2018 sambamba na kudhibiti mianya ya rushwa katika mifumo ya ukusanyaji mapato na utoaji huduma kwa jamii.

Post a Comment

0 Comments