Windows

Tambua faida za mboga ya Spinachi




Naipenda afya yangu na napenda kuhakikisha kila siku ninaupa mwili wangu angalau vitu vinne ambavyo vinamsaada mkubwa katika kuimarisha afya yangu. Vitu hivi ni pamoja na maji ya kutosha, matunda na mboga za majani (chakula bora) na usingizi.

Nina tabia ya ‘kugoogle kila kitu ninachokula ili kufahamu kinafaida gani katika mwili wangu. Yawe matunda, mboga za majani au kitu chochote ambacho nakula kwa wakati huo au kitu ambacho natarajia kwenda kununua kila nipoenda kufanya manunuzi. Na manunuzi yangu mengi ya vyakula huwa nayafanya soko la Kisutu ambalo lina karibu aina zote za mboga za majani na matunda ninayohitaji.

Na mara nyingi nikienda lazima nikute mboga mpya ambayo siifahamu, nikiuliza nikipewa maelezo Naongeza na ‘kugoogle’ halafu nanunua.

Jumapili nilienda kufata baadhi ya mboga na matunda, nikakutana na spinachi nzuri sana. Ile yenye majani mapana, achana na ‘baby spinach’ nikainunua na nikaelezewa faida zake na muuzaji ambaye alikuwa anafahamu kwa undani bidhaa yake. Na leo nimeamua kukushirikisha faida hizo ambazo unaweza kuzipata katika aina yoyote ya spinanchi:

Husaidia kuimarisha afya ya ngozi

Spinachi inapotasiam kwa wingi, viatamini E na vitamin C ambazo zinasaidia kuimarisha afya ya ngozi. Husaidia pia kuilinda ngozi na mionzi ya jua kwa watu ambao tunapigwa na jua kwa muda mrefu katika shughuli zetu za kila siku.

Husaidia kutibu shida mbalimbali ambazo zinahusiana na ngozi ikiwa ni pamoja na chunusi, makovu ya chunusi na shida nyingine. Hii itaweza kusaidiwa kwa kunywa maji ya kutosha kila siku.

Husaidia kuimarisha afya ya macho

Spinanchi ina beta-carotene kwa wingi ambayo husaidia macho kuona vizuri, pia huzuia upungufu wa vitamin A ambayo inahitajika kwa wingi kwa afya ya macho.

Husaidia kuzuia muwasho wa macho au hata kuvimba kwa macho kutokana na uwepo wa virutubisho vingi katika spinanchi. Pia kama una tatizo la kuona wakati wa usiku spinachi itakusaidia kupunguza tatitizo hili kama utaiongeza katika milo yako ya kila siku.

Husaidia kuganda kwa damu.

Wakati mwingine unaweza kuona umejikata sehemu ndogo tu lakini damu inatoka kwa kiasi kikubwa na huchelewa kuacha. Hii ni dalili ya upungufu wa vitamin K ambayo husaidia kugadisha damu hasa wakati ukiwa umeumia. Kula spinach kwa wingi kutasaidia hali hii kupungua au kuacha kabisa.

Huimarisha afya ya mifupa

Spinanchi ina kiasi kingi cha madini ambayo yana faida nyingi mwilini. Madini hayo ni pamoja na potasiam, chuma, manganizi, zinki na copper. Madini haya husaidia kuimarisha mifupa na meno ya mtumiaji.

Kama unatatizo la kucha zako kuwa laini sana na kukatikakatika kila mara spinachi inaweza kukusaidia kwa kiasi kikubwa kumaliza tatizo hili.

Spinachi ina kiwango kikubwa cha protini na ndio maana inashauriwa kuliwa kwa wingi ili kuimarisha afya. Protini ni moja ya vitu muhimu sana katika kuimarisha afya ya mwili kwa ujumla. Mwili unapokosa protini huanza kudhoofika na kupoteza nguvu.

Kuna vyakula vingi ambavyo ni chanzo cha protini na spinanchi ni moja ya vyakula hivyo na ndio maana ina ina umuhimu sana katika mwili wako.

Virutubisho vilivyo katika spinachi kusagwa kwa urahisi na kubadilika kuwa amino acid ambayo ni muhimu kwa mwili wa binadamu. Acid hii huimarisha mishipa na husaidia kuponya vidonda kwa haraka.

Protini inayopatikana katika mboga hii husaidia mmeng’enyo wa chakula kufanyika kwa urahisi na hivyo husaidia kupata haja kubwa kwa urahisi na husaidia kutibu kukosa choo.

Inasaidia kutibu na kuzuia kansa

Kansa ni moja ya mgonjwa mabaya sana ambayo yanatesa watu wengi. Inasemekana kuwa ulaji wa Spinachi kwa wingi husaidia kuzuia na hata kutibu ugonjwa huu.

Spinachi ni moja ya mboga ya majani zenye virutubisho vingi sana na ina faida nyingi katika mwili wa binadamu. Kama utaweza kuiongeza katika milo yako kila siku, itakusaidia sana kuimarisha afya yako kwa kiasi kikubwa

Inaweza kuwa siyo mboga yenye radha nzuri sana lakini ina faida nyingi ambazo zitakusadia kupunguza tripu za kwenda kumuona daktari. Na kama wewe ni mmoja wa watu wasiopenda dawa kama mimi basi wakati umefika wa kuanza kuijali afya yako kwa kula vyakula vyenye faida kama hivi

Vyakula bora ni dawa tosha kwa miili yetu. Ulaji wa vyakula vyenye virutubisho vinavyohitajika mwilini kuna kuhakikishia afya bora na hii itakusaidia sana kupunguza kuingiza kemikali nyingi mwilini unapokuwa unaumwa kwa kutumia dawa. Kinga ni bora kuliko tiba! Kula vyakula ambavyo vinaimarisha afya yako na si vinavyodumaza afya yako kama vyakula vyenye mafuta mengi na vyakula vilivyokoborewa.

Mboga hii inaweza kuliwa kwa chakula chochote; iwe ugali, wali, inaweza pia kutumika kungenezea juisi nzito (smoothie)  Ni nzuri pia kutengezea kachumbari, supu ya mbogamboga. Uamzi ni wako tu ni kitu gani unapenda

Post a Comment

0 Comments