C.E.O wa WCB na Msanii wa Muziki, Diamond Platnumz amepata kigugumizi ishu ya kufanya Wasafi Festival Dar.
Diamond amesema kuwa hawezi kutoa kauli yoyote kwasasa kama afanye au asifanye huku akieleza kuwa mpaka wakae na Team aone maoni yao.
"Siwezi kusema kauli yoyoe kama itafanyika au itakuja nyingine Wasafi Festival 2019 kwasababu lazima nikae na Team, Bodi watoe maoni yao kama inafanyika au haifanyiki ila kwa mimi nimewamisi watu wangu wa Dar Es salaam kuwafanyia kitu kikubwa na kiukweli Wasafi Festival ya Dar tulikuwa tumeipania sana," amesema Diamond Platnumz Wasafi Tv.
Disemba 18, 2018, Baraza la Sanaa liliwafungia kutofanya muziki kwa wasanii wawili ambao ni Rayvanny na Diamond Platnumz kwa kutoa wimbo wenye maudhui mabaya ambao kwasasa wamepewa ruksa ya kuendelea na muziki.
0 Comments