Msanii wa Muziki kutoka lebo ya WCB, Rayvanny ameeleza vile anavyojisikia baada ya kufunguliwa na Basata kwa muda usiojulikana.
Rayvanny ameiambia Wasafi Tv amelishukuru Baraza, Wizara na Serikali na wale wote waliokuwa wanatamani wao wafunguliwe.
"Kiukweli unapopata habari nzuri lazima ufurahi, kiukweli nimefurahi sana, kwasababu nilikuwa kwenye situation ambayo ni sintofahamu kiukweli then hivi vitu ndio first time kuviface hivi vitu, niseme tu nashukuru serikali, nashukuru Baraza, Wizara pia nawashukuru na wale waliokuwa wanatamani sisi kufunguliwa," amesema Rayvanny.
Rayvanny pia ameeleza kile alichojifunza baada ya kufungiwa kazi zake za kisanaa " Ni darasa kwamba tunatakiwa kufuata utaratibu zilizowekwa na serikali kwasababu wanatupenda na wanataka kutuona sisi tunafika mbali, lakini hatuwezi kufika mbali kama hatufuati sheria, alisema Rayvanny.
Disemba 18, 2018, Baraza la Sanaa liliwafungia kutofanya muziki kwa wasanii wawili ambao ni Rayvanny na Diamond Platnumz kwa kutoa wimbo wenye maudhui mabaya.
0 Comments