Windows

Spika Ndugai ajibu madai ya Zitto kutishiwa kifo


Spika wa Bunge, Job Ndugai amejibu madai ya Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe alieleza kuwa  ametishiwa kuuawa na mtu aliyemtaja kama Afisa Usalama wa Taifa ndani ya viwanja vya Bunge.

Akizungumzia suala hilo Spika Ndugai kupitia EATV ameeleza kuwa kila Mbunge yupo salama na barua ya Zitto akielezea suala hilo bado haijamfikia zaidi ya kuiona kwenye mitandao.

“Barua haijanifikia, unajua baadhi ya matatizo tunayapata siku hizi tunayakimbizia kwenye
mitandao, inatakiwa niipate rasmi kama ni ya kweli tutayafanyia kazi”, amesema Spika Ndugai.

Aliendelea kwa kusema, 'Wabunge wako salama kabisa, ukisikia mtu mmoja analalamika, wawili
kwenye kundi kubwa, unatakiwa ulifikirie hilo jambo, sio la kudharau hata kidogo, lakini halimaanishi kwamba hapo mahali usalama haupo,".

from MUUNGWANA BLOG

Post a Comment

0 Comments