Madrid, Hispania. Upepo wa Mbwana Samatta kutakiwa kuondoka katika klabu yake ya Racing Genk unazidi kuvuma baada ya mshambuliaji huyo kuhusishwa kutakiwa Real Betis inayoshiriki Ligi Kuu Hispania ‘La liga’.
Kwa mujibu wa gazeti la Mundo Deportivo, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Tanzania amepewa ofa na klabu hiyo yenye maskani yake jijini Seville baada ya kufunga mabao 25 katika mechi 32 za mashindano yote msimu huu akiwa na Genk.
Samatta, 26, amekuwa katika rada za klabu mbalimbali barani Ulaya hivi karibuni amehusishwa na kutakiwa na Middlesbrough na Cardiff City.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa TP Mazembe amefunga mabao 59 katika michezo 144 aliyoichezea Genk tangu alipowasili katika klabu hiyo miaka mitatu iliyopita.
Msimu huu Samatta anaongoza katika orodha ya wafungaji akiwa na mabao 16 katika michezo 21 aliyocheza hadi sasa.
Genk kwa sasa inaongoza ligi kwa tofauti ya pointi 10.
Betis kwa sasa ipo nafasi ya saba katika msimamo wa La Liga baada ya kuchezwa kwa mechi 20.
0 Comments