Windows

Aliyetumbuliwa na Waziri Lugola aendelea na kazi


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamdun ameendelea kutekeleza majukumu ya cheo hicho licha ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola kutangaza kutengua uteuzi wake.

Utakumbuka January 16 mwaka huu Waziri Lugola ametengua uteuzi wa Makamanda wa polisi watatu ambao ni Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamduni, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel Lukula na Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng'azi.

Uteuzi wa Makanda hao ulitenguliwa kutokana makosa mbalimbali ikiwemo kujihusisha na vitendo vya Rushwa kulinda Askari wanaohusishwa katika kusindikiza utoroshwaji wa bidhaa, na madawa ya kulevya.



from MUUNGWANA BLOG

Post a Comment

0 Comments