Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema wamejiandaa kushinda dhidi ya Namungo FC kesho na hawatajali suala la mwiko kama ilivyokuwa kwa Mbao FC ya Mwanza.
Yanga iko ugenini dhidi ya Namungo FC katika mechi ya Kombe la Shirikisho la Azam FC itakayopigwa kesho mjini Namungo.
Namungo FC inaovaa Yanga ikiwa haijafungwa kwenye uwanja wake wa nyumbani. Jambo linaloelezwa kuwa gumu kwa Yanga na Zahera raia wa DR Congo, amesema hata kwa Mbao FC ilikuwa hivyohivyo.
"Tulielezwa kwamba Mbao FC haiwezi kufungwa na Yanga kwenye uwanja wao pale Mwanza, uliona kilichotokea. Huu ni mpira na hauna mambo ya historia.
"Inategemea mmejiandaa vipi na mnataka kufanya nini uwanjani. Tunataka kucheza vizuri na kushinda, hivyo tumejiandaa," alisisitiza.
Yanga ilifanya mazoezi yake ya mwisho leo mjini humo tayari kwa mchezo huo wa kesho na Zahera amesema wanatambua ni mchezo wa mtoano.
Yanga ilifanya mazoezi yake ya mwisho leo mjini humo tayari kwa mchezo huo wa kesho na Zahera amesema wanatambua ni mchezo wa mtoano.
0 Comments