KMC walianza kufunga bao la kwanza dakika ya 30 kupitia kwa Ally Ramadhani lililodumu mpaka dakika ya 60 ambapo Mtibwa Sugar walisawazisha kupitia kwa mshambuliaji wao Kelvin Sabato.
Matokeo hayo yalidumu mpaka dakika 90 ambapo mwamuzi aliamua mikwaju ya penalti ipigwe na KMC wakashinda penalti 4-3 dhidi ya Mtibwa Sugar.
Mtibwa Sugar wanashindwa kulipa kisasi leo mbele ya KMC kwani walinyooshwa kwenye mchezo wa ligi kwa kufungwa bao 1-0 na leo pia wametolewa kwenye michuano ya FA.
0 Comments