

Msanii wa Bongo Flava Rich Mavoko amesema ana mpango wa kufanya wimbo mwingine na Darassa.
Muimbaji huyo amefunguka hayo kwenye mahojiano na The Playlist ya Times FM ambapo ameeleza kuwa uwezo wa Darassa kimuziki bado upo zaidi.
"Nina plan za kufanya kazi na Darassa tumeshakutana na kuongea, kanisikilizisha (wimbo wake) ni noma," amesema Rich Mavoko.
Utakumbuka kuwa Darassa aliwahi kumshirikisha Rich Mavoko kwenye wimbo wake unaokwenda kwa jina la Kama Utanipenda ambao ulitoka mwaka 2016.
from MUUNGWANA BLOG



0 Comments