Windows

Tshishimbi arejea Yanga SC lakini...



Kiungo wa Yanga SC, Papy Kabamba Tshishimbi tayari amerejea nchini akitokea kwao DR Congo alipoenda kutokana na matatizo ya kifamilia.

Hata hivyo licha ya kureja mchezaji huyo amekuwa akifanya mazoezi pekee yake kwa ajili ya kujiweka sawa huku kukiwa na tetesi za kugoma kutokana na malimbikizo ya fedha anazodai timu hiyo.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Yanga SC, Dismas Ten amethibitisha mchezaji huyo kurejea nchini.

“Tshishimbi yupo nchini na alirudi kabla ya Makambo (Heritier), lakini hawezi kuungana na timu kwa sababu hajafanya mazoezi ya kutosha" amesema.

Aliendelea kwa kusema,'kuhusu madai ya kugoma mimi sijui zaidi ila ninachojua alikuwa kwenye matatizo kwao nchini DR Congo, ila mbali na hivyo pia hajaenda na timu Shinyanga,'.



from MUUNGWANA BLOG

Post a Comment

0 Comments