Siku moja baada ya kuuzwa Misri, kiungo Shiza Kichuya ametolewa kwa mkopo.
Kichuya ameuzwa na Simba katika klabu ya Pharco ya Misri ambayo imeamua kumtoa kwa mkopo Enppi inayoshiriki Ligi Kuu Misri.
Kiungo huyo tayari ni mali ya Mafarao hao na atamalizana na Simba wikiendi hii katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba iko nchini Misri kuwavaa wababe wa Afrika, Al Ahly
0 Comments