MSHAMBULIAJI wa Mbao FC, Said Khamis ameweka rekodi yake kwa sasa Bongo akiwa ni mchezaji wa kwanza kuwatungua magolikipa ghali Ligi Kuu Bara, Aishi Manula na Deogratius Munish wote wa Simba.
Khamisi alianza kumtungua Aishi Manula kwenye Uwanja wa CCM Kirumba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao ulikuwa wa kwanza kwa Simba kupoteza msimu huu ukiwa ni mchezo wao wa nne.
Manula alitunguliwa na Khamis kwa mkwaju wa Penalti na kuifanya Simba kuwa timu ya kwanza kubwa kupoteza mchezo wake mapema kwenye Ligi Kuu Bara kabla ya Azam FC na Yanga kupoteza.
Hivi karibuni kwenye michuano ya SportPesa Cup ambayo Simba walikuwa washindi wa tatu, Khamis alimtungua tena mlinda mlango Deogratius Munish kwa penalti yake ya kwanza Uwanja wa Taifa.
Khamis anaweka rekodi yake Bongo kuweza kuwafunga magolikipa wote wa timu moja kwa aina moja ya ufungaji wa bao la penalti akiwa kwenye viwanja viwili tofauti na mashindano tofauti.
0 Comments