Windows

AUSSEMS AMTUMIA MESEJI ZAHERA


KOCHA mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems ya ameweka wazi kuwa akili yake ipo kwenye mambo mawili tu kwa sasa ambayo ndiyo anayapa kipaumbele zaidi kwenye timu yake.

Aussems amesema kuwa licha ya kukabiliwa na mchezo mgumu wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly lakini anachotakiwa ni kuhakikisha anachukua ubingwa wa msimu huu.

Simba imeondoka jana jioni kuelekea Misri kwa ajili ya mchezo wake wa huo wa hatua ya makundi utakaopigwa Februari 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa Borg El Arab uliopo Alexandaria, Misri.

Mbali ya Simba kushiriki Ligi Mabingwa Afrika inakabiliwa na mechi sita za viporo katika Ligi Kuu Bara huku nyuma kwa pointi 20 mbele ya Yanga wanaongoza ligi wakifuatiwa na Azam wenye poi nti 47.

Aussems ameliambia Championi Jumatano kuwa: “Tuna mechi ngumu Misri lakini b ado haiwezi kuwa kigezo cha kutufanya tuache kuangalia ligi ya kuu kwa sababu tunataka kutetea ubingwa wetu bila ya kuangalia nani yupo juu, tutashinda mechi zetu ili kufikia malengo hayo maana tunataka kurudi huku.”

Post a Comment

0 Comments