

Zahera amesema ana video zaidi ya tatu ambazo zinaonyesha mapungufu makubwa ya waamuzi wa Ligi Kuu Bara, lakini hakuna hatua zinazochukuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Kutokana na ukimya wa TFF katika kuchukua hatua, Zahera ameonya atazifikisha video hizo Caf ili kuangalia namna bora ya kurekebisha makosa ya waamuzi wa soka la Tanzania ikiwemo kuwapa mafunzo.
Zahera amelieleza Mwanaspoti kuwa tayari amefanya mawasiliamo na mwakilishi wa waamuzi wa CAF, ambaye ana makazi yake nchini DR Congo ili kuangalia namna ya kuzifikisha na kupata tafsiri sahihi.
“Nina video nne za dakika 90 lengo la kuzituma huko ni kufahamu tafsiri ya uamuzi ambao naona ni tofauti na nchi zingine au kwa sababu kuna makosa mengine ya wazi yanafanywa na marefa, lakini hakuna hatua.
“Hapa nataka kusaidiwa na Caf kama sheria za huku ni tofauti na mimi sizifahamu kabisa kuhusu hili linalofanywa na waamuzi wa soka hasa kwenye Ligi Kuu,” alisema Zahera.




0 Comments