

Sadney alitua nchini kwa ajili ya kufanya majaribio na timu hiyo ambayo yatakuwa ya siku saba kabla kocha wa Simba, Patrick Aussems kutoa uamuzi kuhusu kumsajili au la.
Aussems atampa nyota huyo Sadney siku saba za kufanya majaribio ikiwemo kucheza mashindano ya SportPesa yatakayomalizika Jumapili ya wiki hii.
Sadney atakuwa sehemu ya wachezaji wa Simba ambao watafanya mazoezi kesho jioni kwenye Uwanja wa Boko Veterans.
Baada ya mechi kumalizika alikwenda katika vyumba vya kubadilishia nguo vya Simba akazungumza na makocha wa Simba Aussems na msaidizi wake Adel Zrane.
Baada ya hapo aliwekwa chini ya ulinzi na Mratibu wa timu hiyo Abbas Selemani akimkataza kuzungumza na mtu yeyote.
Baada ya hapo aliingia katika basi la Simba moja kwa moja alielekea hoteli ya Sea Scape alipofikia.




0 Comments