Windows

Rais wa Colombia Ivan Duque ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa

Rais wa Colombia Ivan Duque ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia shambulizi dhidi ya chuo cha polisi katika mji mkuu wa nchi hiyo Bogota na kuua watu 21 na kujeruhi wengine 68.

Shambulizi hilo la bomu lilitegwa katika gari dogo katika chuo cha polisi kusini mwa mji mkuu Bogota.

Rais wa Colombia amelitaja shambulizi hilo kuwa ni kitendo cha kigaidi.

Tangu alipoingia madarakani mnamo mwezi Agosti, Rais wa Colombia Ivan Duque ameongeza mapambano dhidi ya kundi la waasi la aELN na biashara ya madawa ya kulevya.

Colombia imemekuwa ikikabiliwa na vitendo vya migogoro na vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimedumu kwa zaidi ya nusu karne sasa.

Shambulizi hilo lililotokea Alhamisi wiki hii ni shambulizi baya kuwahi kutokea katika mji mkuu wa Colombia tangu mwaka 2003.

from MUUNGWANA BLOG

Post a Comment

0 Comments