

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wapo nyuma kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya AS Vita katika mchezo wa pili wa Hatua ya Makundi Afrika unaochezwa Uwanja wa Martrys.
AS Vita wameanza kuandika bao dakika ya 14 kupitia kwa Jean Makusu na dakika ya 19 kupitia kwa Butoli Bombunga na bao la tatu likifungwa kwa mkwaju wa penalti na Fabrice Ngoma dakika ya 45 baada ya beki wa Simba Pascal Wawa kumchezea rafu mshambuliaji wa AS Vita.
Kwa sasa mpira ni kipindi cha pili ambapo Simba wamekuwa nyuma katika kufanya mashambulizi hali ambayo inawapa ruhusa washambuliaji wa AS Vita kufanya kile ambacho wanakihitaji katika kutafuta matokeo.



0 Comments