Windows

Rais Trump anatarajiwa kukutana kwa mara ya pili na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kukutana kwa mara ya pili na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un mwishoni mwa mwezi wa pili mkutano ambao umepangwa bila kuwekwa wazi kwa makubaliano ya madai ya pande hizo mbili.

Makubaliano ambayo yanaleta mvuatano kwa pande hizi mbili ni kwamba Marekani inaitaka Korea Kaskazini kuachana na mpango wake wa nyuklia na Korea Kaskazini ukitaka kuondolewa vikwazo.
Mkutano huo unatarajiwa kufanyika mwezi Febuari lakini eneo la mkutano huo bado kuwekwa wazi.

Ikulu ya Marekani imesema kwamba Trump amekutana na Kim Yong Chol ambaye ni mpatanishi wa upande wa Korea Kaskazini kuzungumzia juu ya suala la silaha za nyuklia.

Korea Kusini imepongeza uamuzi huo wa mkutano wa pili kati ya viongozi hao wawili na kusema kwamba matarajio yao utakuwa ni mwanzo wa mabadiliko ya kuleta amani katika eneo la Korea.

from MUUNGWANA BLOG

Post a Comment

0 Comments