TIMU ya Mapinduzi Queens ambayo inashiriki Ligi ya Wanawake maarufu kama Serengeti Lite Women's Premier League inapata taabu kutokana na safu yake ya ushambuliaji kushindwa kuwa na makali huku safu ya ulinzi ikiwa ni butu.
Mapinduzi Queens yenye maskani yake mkoani Njombe mpaka sasa imecheza michezo tisa na imefungwa michezo saba huku ikitoka suluhu michezo miwili na ina pointi mbili ikiwa nafasi ya 12 kwenye Ligi yenye timu 12.
Ofisa Habari wa Mapinduzi Queens, Njenjema Barnabas amesema uongozi umeshtukia hilo kutokana na timu kuwa na mwenendo wa kusuasua dawa ya kuwa na matokeo bora inachemka.
"Kwa sasa hatuna namna zaidi ya kupambana kwa hali na mali tupate matokeo Uwanjani, imani yetu ni kwamba tutawapa mashabiki kile ambacho wanakitarajia nacho ni matokeo mazuri.
"Tunashindwa kuleta ushindani kutokana na wachezaji wetu kushindwa kuhimili mikikimiki ya ligi kwa sasa ila hali hii ni ya muda tu tayari dawa ipo jikoni ni suala la muda, mashabiki watupe sapoti," alisema Barnabas.
Mapinduzi Queens leo atakuwa Uwanjani akimenyana na Simba Queens mchezo wao wa 10 utakaochezwa Uwanja wa Sabasaba koani Njombe majira ya saa 10:00 jioni.
0 Comments