LIGI ya wanawake Tanzania maarufu kama Serengeti Lite Women's Premier League inaenelea kwa timu nane kushuka Uwanjani kumtafuta mbabe wa pointi tatu.
Viwanja vinne leo vumbi litatimka kushuhudia msisimko wa Ligi hii ambayo bingwa mtetezi ni JKT Queens.
Evergreen Queens kazini leo uwanja wa Karume kumenyana na Baobab Princess, JKT Queens mzigoni kumenyana na Sisterz FC uwanja wa Mej.Gen.Isamuhyo.
Marsh Queens watamenyana na Mlandizi Queens uwanja wa Nyamagana na Mapinduzi Queens mzigoni leo uwanja wa Sabasaba dhidi ya Simba Queens, mechi zote hizi zitaanza saa 10:00 jioni.
0 Comments