Windows

KIGOGO KIBOKO YA WAARABU ANG’ATUKA SIMBA


KIGOGO wa Simba ambaye aliwahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Kassim Dewji ambaye amewahi kuwa mbabe katika mechi za Waarabu ameamua k u j i w e k a pembeni na soka kwa sasa.

Dewji ni miongoni mwa wadau wakubwa wa mpira hapa nchini ambaye alikuwa mmoja wa viongozi wa kundi la Friends of Simba akiwa pamoja na aliyekuwa Rais wa Simba, Evance Aveva ambaye kwa sasa yupo rumande.

Kigogo huyo wa Simba alikuwa akihusika kwa kiasi kikubwa katika kuiwezesha timu hiyo pamoja na kutoa uhamasishaji kuhakikisha inafanya vizuri katika mechi mbalimbali zikiwemo zile ambazo zilikuwa zikiwahusisha Waarabu.


Dewji alihusika kwa sehemu kubwa kuipa heshima Simba baada ya kuwa kiongozi wa mstari wa mbele kwenye mchezo wa Simba dhidi ya Zamalek mwaka 2003, mchezo ambao Simba walishinda na kuingia hatua ya makundi Klabu Bingwa Afrika.

Hata hivyo katika siku za hivi karibuni kigogo huyo amekuwa haonekani uwanjani kama ilivyokuwa huko nyuma wakati Simba ikicheza.

Championi Jumatano lilimtafuta, Dewji kuweza kutoa maoni yake juu ya mwenendo wa timu kuelekea katika mchezo wake dhidi ya Al Ahly ya Misri katika mechi itakayochezwa Jumamosi ijayo ambapo alieleza wazi juu ya kuachana na soka.

“Kwa sasa mimi sina ushauri wala maoni yeyote kwa Simba nimeshaachana na masuala ya soka muda mrefu sasa na wala sifuatilii wala sijui kinachoendelea kwa sasa ndugu yangu,” alisema na kukata simu.

Post a Comment

0 Comments