Windows

KOCHA SIMBA AMUONGEZA KIKOSINI MMOJA WA KIMATAIFA


Kocha wa Simba, Patrick Aussems raia wa Ubelgiji amefunguka kuwa kama akiamua kumsajili mchezaji mmoja kwa sasa ndani ya kikosi hicho anamfikiria zaidi straika Mnamibia Sadney Urikhob kwani ni mchezaji ambaye ana vitu tofauti na wachezaji alionao ndani ya kikosi hicho.

Kwa sasa Simba ina wachezaji wane ambao wanafanya majaribio ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya kupewa mkataba.

Wachezaji hao ni beki, Lamine Moro, kiungo Jean Bitar Ourega raia wa Ivory Coast pamoja na washambuliaji Hunlede Kissimbo na Urithob.

Kocha huyo amesema kuwa anaendelea kumuangalia kila mchezaji kwenye mazoezi ya kikosi hicho lakini anamfikiria zaidi Urithob kwani uwezo wake utaongeza kitu kwenye kikosi chake.

“Wote ninaendelea kuwaangalia kila siku kwenye mazoezi yetu, ninaangalia kila mmoja namna anavyojituma uwanjani na pia jinsi anavyotoa msaada kwetu.

“Ila nadhani kama tukiamua kumchukua mmoja basi straika Mnamibia anafaa kwani ana kitu ambacho anaweza kukiongeza ndani ya timu yetu na tukaongeza makali hasa kwenye eneo letu la ushambuliaji,” alisema kocha huyo.

CHANZO: CHAMPIONI

Post a Comment

0 Comments