Windows

KOCHA AZAM AJA NA MBINU ZA KUWAUMIZA SIMBA NA YANGA


KOCHA Mkuu wa Azam FC, Hans Pluijm amesema kikubwa ambacho anafikiria ni kupata matokeo yatakayoisaidia timu yake kutwaa kombe la Ligi Kuu Bara huku akiipigia hesabu nafasi ya kwanza iliyo mikononi mwa Mwinyi Zahera.

Azam wanashika nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 20 na Yanga wanashika nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 53 tofauti ya pointi sita ambazo ni sawa na michezo miwili.

Akizungumza na Championi Jumatano, Pluijm alisema kuwa kwa sasa anapasua kichwa namna ya kupata matokeo chanya yatakayomsaidia kushika nafasi ya kwanza ili afikie malengo ya timu.

"Wachezaji wanapambana wakiwa Uwanjani kupata matokeo, nina amini wakati utafika na tutarejea nafasi ya kwanza kwa kuwa kwenye mpira kila kitu kinawezekana na suala la kuongoza ni muda tu.

"Kwa sasa nimewaambia wachezaji wangu tunatakiwa kupata matokeo chanya kwenye michezo yetu inayofuata tunatambua ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji matokeo tuna nafasi ya kufanya vizuri," alisema Pluijm.


Post a Comment

0 Comments