

Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini, Nay wa Mitego amefunguka sababu ya yeye kusitisha kuonesha mali zake anazomiliki ni kutokana na kukatazwa na mama yake.
Nay amesema kuwa mwanzo alikuwa anaonesha magari, nyumba, na biashara zake kwasababu mama yake hakuwa akijua, lakini alipokuja kugundua alimpiga 'Stop'.
"Mimi nimeacha hivyo vitu, huwa namsikiliza sana bi mkubwa wangu (mama), alikuwa hajuagi mambo ya mitandaoni lakini ilifika 'time' kuna mtu akaenda kumuonesha baadhi ya vitu akaniambia "no mimi sipendi hivi Kama una kitu na unataka kuoneakana basi kawatolee watu", amesema Nay.
Nay ameachia wimbo wake mpya wiki hii unaojulikana kwa jina la "Mbele kwa mbele" na unaonekana kupokelewa vizuri na mashabiki wa muziki wake.
from MUUNGWANA BLOG



0 Comments