Windows

kuainisha maeneo kwa ajili ya utalii wa Fukwe


Wizara ya Maliasili na Utalii, imeanza kuyatambua na kuainisha maeneo kwa ajili ya utalii wa Fukwe katika Kisiwa cha Mafia mkoani Kibaha kwa ajili ya kuhamasisha Wawekezaji kuchangamkia fursa ya ujenzi wa Hoteli za kitalii ili kuwavutia watalii kutembelea katika kisiwa hicho.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa aliyoyatoa mwaka jana kwa Wizara hiyo  kuwa ianzishe Kurugenzi ya Fukwe itakayokuwa na jukumu la kusimamia na kuendeleza  Fukwe zote nchini.

 Lengo likiwa ni kuhakikisha mapato yatokanayo na sekta ya Utalii kupitia Utalii wa Fukwe yanaongezeka kwa mfano Kisiwa cha Mafia ni cha tano duniani kwa uzuri wa vivutio vya utalii na rasilimali bahari na  cha pili barani Afrika, Hivyo kina sifa kemkem za kuongeza pato la Taifa zaidi.

Akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya siku mbili kisiwani humo ya kutembelea Fukwe pamoja na magofu ya kale,  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu  amesema Wizara imejipanga kikamilifu kwa ajili kuwasaidia  Wawekezaji wenye nia ya kuwekeza kwenye Fukwe kwa ajili ya utalii.




from MUUNGWANA BLOG

Post a Comment

0 Comments