Windows

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi DAWASA atembelea mtambo wa uzalishaji Maji


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA), Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange ametembelea mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu Chini na kushiriki upandaji wa miti pembezoni mwa chanzo cha Mto Ruvu.

Mwamunyange amepanda mti sambamba na wajumbe wa bodi kwa ajili ya kulinda vyanzo vya maji vya mto Ruvu ikiwa ndio chanzo kikubwa kinachozalisha maji kwa asilimia 88 katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.Akiwa katika ziara yake ya siku ya pili, Mwamunyange ametembelea mtambo huo ikiwa ni mara ya kwanza toka achaguliwe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo.

Pia ametembelea mtambo huo akiwa ameongozana na wajumbe wa bodi ya DAWASA kuona namna uzalishaji maji unavyoanzia na kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa wahandisi wa Mamlaka hiyo.Akizungumza baada ya kumaliza kutembelea mtambo huo, Mwamunyange amesema kiwango kikubwa cha uwekezaji kimefanyika na wataalamu wanafanya kazi kubwa kuhakikisha wananchi wanapata maji.

Hata hivyo amesema jitihada kubwa za serikali zinafanyika kuhakikisha wananchi wote wanapata maji hususani kwenye maeneo yaliyokuwa hayana maji kwa kipindi chote kikubwa wananchi wawe wavumilivu kwakuwa DAWASA wanafanya kazi kuwapelekea maji.Baada ya kuwasili katika mtambo huo Mwamunyange alipata fursa ya kuzungumza na wafanyakazi wa mtambo huo na kuwataka wafanye kazi kwa juhudi kubwa ili kutimiza adhma ya serikali ya kufikia asilimia 95 ya wananchi wote ifikapo 2020.






from MUUNGWANA BLOG

Post a Comment

0 Comments