Windows

JIKUMBUSHE TAMATI MICHUANO YA SPORTPESA CUP NA UBINGWA KARIAOBANGI SHARKS




Baada ya wiki moja ya kuvutia kwa mashabiki wa mpira wa miguu kwenye Ukanda huu wa Afrika Mashariki ya SportPesa Cup ambayo ilileta pamoja timu nane kutoka KENYA na Tanzania (Kariobangi Sharks, Bandari FC, AFC Leopards, , timu ya Kariabangi Sharks kutoka Kenya imetangazwa kuwa bingwa wa michuano hiyo kwa mara ya kwanza.

Michuano hiyo ambayo ilianza tarehe 22 Januari kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ilikuwa ni maalum kwa wachezaji pamoja na makocha kama ambavyo ilivyoelezwa na Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania Tarimba Abbas ambaye alisema, ‘Michuano hii ni muhimu na maalum kwa wanafamilia wa mpira wa miguu kwani inatoa fursa kuonyesha vipaji vyao. 

Vile vile kwa timu bora kutoka Kenya na Tanzania kucheza pamoja, ilikuwa ni muda wa kuonyesha vipaji vya mpira Barani Afrika na kukuza mchezo huo kwenye Ukanda huu.

Balozi wa Kenya nchini Tanzania Dan Kazungu alisema kuwa michuano hiyo ambayo ilikuwa ni awamu ya tatu imekuwa na umuhimu mkubwa wa kukuza uhusiano kati ya nchi hizi mbili. ‘Kwa sisi kama ubalozi, tunachukulia michezo kama fursa ya kuleta watu wetu pamoja alisema huku akiongeza kuwa wakati ambapo Kenya na Tanzania wanapokuja pamoja kwenye michezo huku jamii pia ikija pamoja na kushangalia kwa furaha inakuwa inaongeza na kukuza umoja wa jumuiya yetu.

Michuano hii imekuwa ni hatua kwa wachezaji kufikia malengo yao wakiwepo wachezaji wa Gor Mahia Meddie Kagere na beki Godfrey Walusimbi kuvutia timu zingine baada ya kuonyesha ubora wa viwango vyao kwenye awamu ya pili ya michuano ya SportPesa Cup. Kwa sasa Kagere anachezea klabu ya Simba SC huku Walusimbi akichezea Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini. 


 Michuano hio pia imeudhuriwa na mchezaji wa zamani wa Klabu ya Everton FC na timu ya Taifa ya Afrika Kusini Steven Pienaar, ambaye alifurahishwa na viwango vya wachezaji kwenye michuano hiyo. Wakati wa ziara yake, mchezaji alishiriki kwenye kugawa vifaa vya michezo kupitia kampeni ya ‘Kits for Africa’ yenye lengo ya kuwafaidisha zaidi ya wachezaji chipukizi 200. Kwa msimu huu, SportPesa imeweza kukusanya vifaa zaidi ya 45,000 ambavyo zvtagawiwa kwenye nchi za Kenya, Tanzania na Afrika Kusini.

Pienaar alisema, ‘Ilikuwa ni furaha kuona ni kwa jinsi ngani ushirikiano baina ya SportPesa na Everton umekuwa na umuhimu kwa jamii ambayo inaishi kwenye mazingira magumu hapa Tanzania. ‘Kits for Africa’ ni moja tu ya kampeni ambayo SportPesa imekuwa ikiendesha ili kukuza fursa ya vipaji vya baadae hapa Afrika Mashariki.

Bingwa mpya wa michuano ya SportPesa Cup, Kariobangi Sharks, kwa sasa wanarudi nchi Kenya na kuendelea kwenye ligi ya nchi hiyo ambapo kesho watacheza na timu ya Mathare United kwenye uwanja wa Moi Sports Centre, Kasarani saa tisa jioni.






Post a Comment

0 Comments