Zahera amesema wachezaji wake ni wapambanaji wakiwa ndani ya Uwanja hivyo kila mchezaji anapokuwa akisumbuliwa na majeruhi huwa anaumiza kichwa kujua nani ataziba nafasi yake hivyo anakuwa kwenye wakati mzuri wachezaji wake wanapokuwa fiti.
"Kurejea kwa wachezaji Raphael Daud na Juma Mahadhi kunaongeza upana wa kikosi ambacho kitapambana na wapinzani wetu kwenye mchezo wetu wa FA dhidi ya Biashara United.
"Kwa sasa nitakuwa nacheza nikiwa na wachezaji wangu wote muhimu hasa baada ya kurejea kwenye kikosi, mchezo wetu dhidi ya Biashara kesho utakuwa mgumu ila tutapambana kutafuta matokeo," alisema Zahera.
Yanga watacheza kesho Uwanja wa Taifa dhidi ya Biashara United majira ya saa 10:00 ikiwa ni mchezo wa FA raundi ya nne.
0 Comments