KESHO Uwanja wa Taifa majira ya saa 10:00 jioni kikosi cha Yanga kitashuka Uwanja wa Taifa kumenyana na Biashara United ikiwa ni mchezo wa raudi ya nne kombe la Shirikisho.
Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema morali kwa wachezaji ni kubwa ila watawakosa wachezaji wawili wa kikosi cha Yanga ambao ni majeruhi.
"Wachezaji wetu wote wapo na morali ya kupambana, ila wachezaji wetu wawili ambao ni Jafary Mohamed na Baruan Akilimali wataokosa mchezo wa kesho.
"Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu yao tunawaheshimu wapinzani wetu na tunajua utakuwa ni ugumu ila hesabu zetu ni kupata matokeo," alisema Saleh.
0 Comments