Windows

FREDY MINZIRO AKUBALI YAISHE NA UONGOZI WA ARUSHA UNITED


LICHA ya kuiongoza timu yake kushika nafasi ya tatu kwenye mzunguko wa kwanza bado amefungishiwa virago na uongozi wa Arusha United inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza na amekubali yaishe kiungwana.

Fredy Minziro ambaye msimu uliopita aliipandisha timu ya KMC Ligi Kuu na alitemwa kabla ya Ligi kuanza akiwa na mikakati yake kibao yamekuta tena hata kabla hajatimiza mipango yake Ausha United.

"Mzunguko wa kwanza nimekamilisha na kikosi changu niliweza kukiweka nafasi ya tatu kwenye msimamo sijajua tatizo lipo wapi kwa sasa, ila hamna namna kwa kuwa wameamua wao napokea uamuzi wao, ila nina uwezo na uzoefu kwani nimepandisha timu ya Singida United, KMC zote zinashiriki Ligi Kuu.

"Viongozi wangu wenyewe wameona kwamba sina mwenendo mzuri na wameamua kumleta kocha mpya Hemed Morroco ili apambane hivyo huenda atabadilisha matokeo," alisema Minziro.

Post a Comment

0 Comments