Windows

Baada ya 'Nyegezi' kufungiwa, Diamond na Rayvanny warudi studio, Lava Lava akaribishwa


Mara baada ya kuondoleWa adhabu na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA), msanii Diamond Platnumz na Rayvanny ameelezea furaha yao.

Wasanii hao kutokea WCB wameingia studio kurekodi wimbo mwingine mara ya wimbo wao wa mwisho kutoa 'Mwanza' kufungiwa.

Katika wimbo huo mpya kuna uwezekano mkubwa Lava Lava naye akashirikishwa kutokana aliambatana nao.

Katika video ambayo Diamond ameiweka kwenye mtandao anamtaja Lava Lava pia ingawa hajaeleza moja kwa moja kama atahusika.

Huo utakuwa ni wimbo wa nne kwa Diamond kufanya na Rayvanny baada ya Salome, Iyena na Mwanza. Nyimbo nyingine walizofanya wote na wasanii wengine ni kama Zilipendwa (WCB) na Fresh Remix (Fid Q).



Post a Comment

0 Comments