

Msanii wa Filamu Bongo, Elizabeth Michael Lulu ameeleza sababu ya kutangaza kugawa nguo zake.
Mrembo huyo kutoka kiwanda cha filamu ametumia mtandao wa Instagram ambapo ameeleza kuwa nguo hizo hatozitoa bure bali kwa fedha na kiasi kitakachopatikana kitaenda kuwasaidi watoto
yatima.
"Kuelekea siku ya Wapendanao Februari 14,Nimeamua Kuuza Sehemu Ya Nguo Zangu Ambazo Yawezekana Umeshawahi Kuziona au Haujaziona. Na Pesa Yote Itakayopatikana Kupitia Mauzo Haya Itaenda Kusaidia Vitu/Watu Wenye Uhitaji Katika Jamii," ameeleza Lulu.




0 Comments