Windows

Madiwani wa Halmashauri ya Tarime wapitisha bajeti ya shilingi Bilioni 24.1


Na Timothy Itembe Mara.

Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara jana wamepitisha Bajeti ya shilingi Billioni 24149231375 ikiwa ni mapata na matumizi ya halmashauri katika mwaka wa fedha 2019/2020.

Akifafanua Bajeti hiyo kwenye baraza hilo Afisa mipango wa halmashauri hiyo,Belton Garigo kwa niaba ya mkrugenzi wake,Elias Ntiruhungwa alisema kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020 halmashauri inaomba kuithinishiwa na kukusanya jumla ya shilingi 24149231375.30 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia8.85 ya bajeti ya mwaka 2018/2019 iliyoithinishwa na Bunge.

Garigo aliongeza kuwa ongezeko hilo linatokana na bajeti ya miradi ya maendeleo kufuatia maandiko ya miradi ya kutolea huduma(Servuce  Delivery Projects) na ujenzi wa wa ofisi ya makao makuu ya halmashauri ya Mji wa Tarime.

"Mwongozo wa kuandaa mpango wa Bajeti ya mwaka 2019/2020 pamoja na maelekezo mahususi kwa mamlaka za mitaa umetuelekeza kuandaa na kuwasilisha maandiko ya miradi ya kutolea huduma(Service Ddelivery Projects) kutokana na frusa hiyo halmashauri ya Mji wa Tarime imeandaa maandiko Manne na kuwasilisha Wizara ya Fedha"alisema Garigo.

Garigo alitaja maandiko hayo kuwa ni pamoja na ujenzi wa vyumba 12 vya madarasa katika shule za sekondari Sabasaba vyumba 4Tagota vyumba 4 Nkongore vyumba 4 pamoja na ukamilishaji wa maabara 18 katika shule za sekondari Bomani vyumba 3 Nyamisangura vyumba 3 Kenyamanyori vyumba 3Nkende vyumba 3 Rebu vyumba 3 na Nyandoto vyumba 3 kwa garama ya shilingi 872763160.

Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Elias Ntiruhungwa alisisitiza kuwa halmashauri yake imejipanga kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza ifikapo mwezi Februali  2019 wanaanza masomo kama ilivyopangwa kutokana na halmashauri hiyo kwa kushirikiana na jamii kukamilisha vyumba vya madarasa na kuondoa uhaba uliopo.

Katika hatua nyingine halmashauri imejipanga katika ujenzi wa vyumba 16 vya madarasa katika shule za msingi Mtingilo vyumba 4Mwibari vyumba 4,Nchora vyumba 4 na Taramoroni vyumba 4 kwa garama ya shilingi 400,000,000 pamoja na ukamilishaji wa ujenzi wa kituo cha Afya Magena kwa kujenga jengo la OPD Word ya wanawake na wanaume,chumba cha XRAY,uzio,kichoma taka,njia ya wagonjwa na jiko kwa garama ya shilingi 392,000,000 huku halmashauri hiyo ikikamilisha ujenzi wa kituo cha Afya Kenyamanyori kwa lengo la kuwapunguzia umbali Wananchi kwenda katika Hospitali ya wilaya na kupunguza mlundikano wa Wagonjwa katika  kituo kimoja kwa garama ya shilingi 792,000,000 aliongeza Ntiruhungwa.

Katika kikao hicho mwenyekiti wa halmashauri ya Tarime Mjini,Khamisi Nyanswi Ndera kupitia Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema aliwataka watumishi pamoja na madiwani kutoa ushirikiano ili bajeti iliyokasimiwa kwaajili ya maendeleo kutumika kwa utekelezaji kama iivyo pangwa.

Nyanswi alitumia nafasi hiyo kuwataka madiwani kujitoa kwa moyo kuwatumikia wananchi kwasbabu waliwachagua huku wakiwaamini kuwapa nyadhifa waliyo nayo.

Post a Comment

0 Comments