

Leo Rais wa Jahmuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na viongozi mbalimbali wa Dini Ikulu Dar es Salaam na kuongea nao.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima alipata nafasi ya kusimama na kuongea mbele ya Rais Magufuli.
’Pale Airport Dar es Salaam kuna mahali pa kuabudia kwa Waislamu, lakini mahali pa kuabudia
kwa Wakristo hakuna, kwa hiyo iangaliwe kwa kuweka kumbukumbu, wote wanahitaji," amesema Akofu Gwajima.
Aliendelea kwa kusema, 'Nakupongeza umefanya jambo ambalo halijawahi kutokea kwenye historia, tumekuja pamoja leo hapa kwa upendo kujadili mambo yanayohusu nchi yetu,'.




0 Comments