Uongozi wa Yanga umepanga 'kuwakata' nyota wa kigeni ambao wameshindwa kuonyesha makali kwenye timu hiyo
Baadhi yao tayari wametaarifiwa huku wengine wakiomba wenyewe mikataba yao ivunjwe
Wachezaji kigeni waliosajiliwa dirisha lililopita ni Farouk Shikhalo, Mustafa Suleyman, Lamine Moro, Patrick Sibomana, Issa Bigirimana, Maybin Kalengo, Juma Balinya, Sadney Urikhob na David Molinga
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema taarifa kamili itatolewa baada ya kumalizika michakato ya ndani
Aidha Bumbuli amesisitiza kuwa wametoa mapumziko ya siku tatu kwa wachezaji wote wa kikosi cha kwanza kutokana na kusimama kwa ligi
Pia amesema makocha na baadhi ya wachezaji waliomba kushiriki msiba wa Ally Yusuf ‘Tigana’
Nyota wa kigeni waliruhusiwa kusafiri kwenda kusalimia familia zao
0 Comments