Klabu ya Yanga inatarajiwa kuongeza nyota wanne dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa wiki ijayo, Disemba 16 2019, imefahamika
Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Ufundi amesema watawasilisha mapendekezo ya usajili kwa Kamati ya Utendaji katika kikao kitakachofanyika wikiendi hii
"Mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya Ufundi ni kusajili wachezaji wanne, beki wa kushoto, beki wa kati, kiungo mshambuliaji na mshambuliaji wa kati mmoja"
"Majina ya wachezaji hao tunayo, tutayawasilisha kwenye kikao na Kamati ya Utendaji ambacho kitafanyika kesho (leo)," alisema
Yanga imedhamiria kukamilisha mapema usajili wa nyota hao ili kama ikiwezekana wawatumie kwenye mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa January 04 2020
Baada ya dirisha la usajili kufunguliwa Disemba 16, Yanga itakuwa na takribani siku 18 kuhakikisha inapata vibali vya nyota wa kigeni ambao watasajiliwa ili kuwawezesha kucheza mchezo dhidi ya Simba
Hata hivyo hatma yao itategemea kufanyika kwa kikao cha TFF kuidhinisha usajili wa dirisha dogo kwani kama kikao hicho kitafanyika baada ya dirisha la usajili kufungwa, wachezaji hao hawataweza kutumika kabla ya wakati huo
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.
0 Comments