Na EMMANUEL MBATILO
Klabu ya Simba imependekezwa kucheza mechi dhidi ya timu ya Sevilla ya nchini Hispania hasa kutokana na matokeo mazuri waliyoyapata katika mashindano ya Sportpesa.
Mwanzo timu mbili kutoka Tanzania yaani Yanga na Simba zilitakiwa kucheza ili kutafuta mshindi ambaye ataweza kuumana na timu ya Sevilla lakini kutokana na ratiba ya ligi kuwa ngumu, Shirikisho la mpira wa miguu pamoja na Sportpesa wakakubaliana yakuwa Simba itacheza na Sevilla.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Katibu mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Kidao Wilfred amesema kuwa wao kama wasimamizi wa mpira wa miguu hapa nchini wameona ni hatua kubwa kwa timu kama Sevilla kuja hapa nchini kucheza mechi na timu ya hapa, ndo maana wakaamua kufanya maamuzi ambayo yanaweza kuwasaidia hasa kutokana na hali halisi ya ligi kuu Tanzania bara.
“Katika mashindano ya Sportpesa yaliyoisha hivi karibu timu ambayo kwa Tanzania ilifanya vizuri kuliko timu nyingine ilikuwa klabu ya Simba kwahiyo tunatangaza rasmi yakuwa klabu ya Simba itacheza na Sevilla Mei 23 mwaka huu “. Amesema Kidao.
Aidha Kidao ameongeza kuwa Sportpesa waliwaandikia barua ya kuomba createria ambazo Tff watazitumia kama wasimamizi wa mpira wa miguu kupata timu ambayo itacheza na Sevilla bila kuathiri ratiba ya ligi na kalenda kwa ujumla.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti Sportpesa, Bw.Tarimba Abbasi amesema kuwa suala la timu ipi icheze na Sevilla limekuwa likiwaumiza na wamekuwa wakifikilia kwamba njia pekee ambayo ingeweza kuondoka mzizi wa fitina ni kucheza kwa timu mbili yaani Simba na Yanga ili kupata mshindi ambaye atacheza na Sevilla.
“Ratiba tumeiangalia mara nyingi tukisema hapa wanasema hapana haikuwa inawezekana hata siku moja mechi kati ya Simba na Yanga kucheza”. Amesema Bw. Abassi
Hata hivyo Bw.Abbasi ameongeza kuwa hata kama Sevilla wanaileta wao lakini ni lazima wapewe ushirikiano kutoka shirikisho la mpira wa miguu Tanzania.
0 Comments