Kesho Jumatatu kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuelekea mkoani Mbeya tayari kwa michezo miwili ya ligi kuu dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons
Keshokutwa Jumanne, Disemba 24 Yanga itacheza na Mbeya City katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Sokoine kisha kuwavaa Tanzania Prisons katka mchezo mwingine ambao utapigwa Disemba 27
Wanachama wa klabu ya Yanga mkoani Mbeya walikutana jana kuweka sawa mapokezi ya timu yao
Mkutano huo uliongozwa na Mwenyeki wa Mkoa Chuma Mahinya akiwa na mgeni kutoka Makao Makuu Saad Khimji ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji
Katika Mkutano huo, Wanachama walichanga pesa taslim Tzs 1,010,000/= huku kiasi cha Tzs 405,000/- zikiwa ahadi
Wanachama wa Matawi nao wamechanga Tzs 975,000/=
0 Comments