Uongozi wa klabu ya Yanga umeachana na mpango wa kumsajili beki wa Coastal Union na timu ya Taifa Bakari Nondo Mwamnyeto baada ya kumrejesha beki wake kisiki Andrew Vicent 'Dante', imefahamika
Juzi Yanga ilitangaza kumalizana na Dante na mchezaji huyo kuingia kambini kuendelea na maandalizi ya michezo ya ligi na michuano mingine inayofuata
Inafahamika Yanga ilikuwa mbioni kumsajili Mwamnyeto, kulikuwa na majadiliano baina ya viongozi wa Coastal Union na Yanga juu ya dau la usajili wa mchezaji huyo
Lakini kurejea kwa Dante kumefuta mpango huo kwani mabingwa hao wa kihistoria hawana tena sababu ya kuongeza beki, wana walinzi sita wa kati
Kelvin Yondani, Andrew Vicent, Mustafa Suleyman, Lamine Moro, Ally Mtoni na Ally Ally wote ni walinzi wa kati
0 Comments