Windows

Yanga imeniongezea kujiamini - Balama



Kiungo anayekuja kasi Tanzania Mapinduzi Balama amesema usajili wake Yanga umekuwa na manufaa kwake

Balama aliyesajiliwa na Yanga mwezi Juni akitokea klabu ya Alliance Fc, amesema ushiriki wake katika mechi za Kimataifa na kikosi cha Yanga umemuongezea kujiamini

"Tangu nisajiliwe Yanga kutokana tumecheza mechi nyingi za Kimataifa, kwa kweli nimeongeza kujiamini"

"Sasa hivi sihofiii kucheza mechi yoyote itakayokuja mbele yangu," amesema Balama

Aidha kiungo huyo fundi amesema wanafahamu wanakabiliwa na michezo migumu mkoani Mbeya dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons lakini wamefanya maandalizi ya kutosha hivyo wana matumaini ya kufanya vizuri

Balama amekuwa na kiwango kizuri tangu alipojiunga na mabingwa hao wa kihistoria mwanzoni mwa msimu

Nyota huyo anaunda safu ya kiungo ambayo itamjumuisha Haruna Niyonzima aliyesajiliwa hivi karibuni

Papy Tshishimbi, Abdulaziz Makame, Mohammed Issa 'Banka', Feisal Salum, Raphael Daudi na Said Juma ni nyota wengine wanaounda safu hiyo

Post a Comment

0 Comments