Windows

Tukio la nyuki kuvamia uwanja wa Uhuru gumzo





Jana hali haikuwa shwari ndani ya Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam katika mchezo kati ya Yanga na Iringa United wa Kombe la Shirikisho baada ya kundi kubwa la nyuki kuvamia uwanjani hivyo kuleta taharki kwa wachezaji, wamauzi na mashabiki.

Kundi hilo la nyuki lilipita uwanjani dakika ya 53 na kuwafanya wachezaji wa timu zote mbili pamoja na waamuzi kulala chini.

Baada ya wachezaji kulala, beki wa Yanga Ali Mtoni Sonso alionekana kunyanyuka ghafla huku akijikung'uta kichwani akiashiria kung'atwa na wadudu hao hivyo kukimbia nje kwenye benchi la timu yao ili kpata huduma ya kwanza.

Nyuki hao hawakuishia uwanjani tu kwani walienda mpaka katika baadhi ya majukwaa na kusababisha mashabiki kulala chini na wengine kukimbia kujiokoa.

Tukio hilo lilidumu kwa dakika sita na dakika ya 59 mwamuzi aliashiria mchezo kuendelea baada ya hali kuwa sawa na nyuki hao kutokomea

Wakati huo nyuki wakivamia uwanja Yanga walikuwa mbele kwa mabao 3-0 katika mchezo huo ambao waliibuka na ushindi wa mabao 4-0

Baadhi ya mashabiki wamelihusisha tukio hilo na imani za kishirikina kuwa watani zao Simba 'walitia mkono' kutaka kuwavurugia

Hata hivyo mpango huo ni kama ulichelewa kwani muda ambao nyuki hao walivamia, ushindi tayari ulikuwa njiani!

Post a Comment

0 Comments