Windows

Huyo straika mpya Yanga vichwa anafunga ,chini pia hakuachi




Jana kabla ya swala ya Ijumaa, bilionea huyo ameshusha straika mmoja mrefu ambaye kama atamalizana na klabu hiyo kisha kusaini, Simba inabidi wajipange katika kumdhibiti, nunueni ngazi ili muweze kumdhibiti akitokea klabu moja kubwa ya nchini humo.ADVERTISEMENT
By Khatimu Naheka


KWA kimo alichonacho ni kama Peter Croach ama Andy Carroll waliokimbiza sana pale England na kwa misuli minene aliyonayo straika mpya aliyeletwa jana Ijumaa na Yanga kwa ajili ya kumsainisha ni wazi, mabeki wa timu pinzani wajipange tu.


Akiwa na urefu wa zaidi ya futi sita, Yikpe Gislain Gnamian ni wazi wachezaji na mabeki wa pembeni wa Yanga watakuwa na kazi ya kupiga krosi za juu ili jamaa awe anamalizia tu nyavuni kwa kichwa.


Ipo hivi. Bilionea wa Yanga, wala hana mpango wa kufunga zipu ya begi lake la fedha kwani, unaambiwa jamaa kwa sasa akitoka nchi hii anaingia nyingine, kwani baada ya kutoka Uganda kisha Rwanda kwa sasa ameacha kilio Kenya kwa kuvuta straika mmoja ngongoti ili kumaliza ukame wa mabao.


Jana kabla ya swala ya Ijumaa, bilionea huyo ameshusha straika mmoja mrefu ambaye kama atamalizana na klabu hiyo kisha kusaini, Simba inabidi wajipange katika kumdhibiti, nunueni ngazi ili muweze kumdhibiti akitokea klabu moja kubwa ya nchini humo.


Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere III, straika Gnamien Gislain Yikpe alitua rasmi kama ambavyo Mwanaspoti jana lilivyokupa likiwa gazeti pekee lililokuwa linajua ujio wake.


Gnamien, raia wa Ivory Coast ametua saa 5 asubuhi na kupokewa na Mkurugenzi wa Mashindano ya Yanga, Thabit Kandoro tayari kwa maongezi na hata kuangaliwa kidogo kabla ya kusainishwa mkataba.Ujio wa Gnamien inaelezwa ni ushawishi wa bosi mmoja wa juu wa klabu hiyo na haraka wadhamini wa klabu hiyo GSM kupitia Bilionea wao, Ghalib Mohamed aliyeamua kusimamia usajili kamili akamleta nchini akimtumia Mhandisi, Hersi Said anayezunguka nchi kadhaa kuleta vifaa vipya.


Mara baada ya kutua jana hiyo hiyo straika huyo alifika moja kwa moja kambini kuungana na wenzake na leo wanacheza mchezo wa Kombe la FA dhidi Iringa United ya Ligi Daraja la Kwanza katika Uwanja wa Uhuru.




REKODI YAKE SASA


Straika huyo mrefu, inayeelezwa amezaliwa miaka zaidi y 24 iliyopita, alisajiliwa na Gor Mahia Julai mwaka huu kwa ajili ya msimu huu wa Ligi Kuu Kenya, akitokea Gagnoa FC iliyopo Ligi Kuu ya Ivory Coast alikoifungia mabao matano.


Hata hivyo, kabla ya kuichezea Gagnoa ya kwao Ivory Coast, straika huyu msimu wa 2017-2018 akiwa Hafia FC ya Ligi Kuu ya Guinea, alitupia kambani mabao manane kuonyesha jamaa ni fundi wa kutupia.


Katika muda mfupi aliokaa na Gor Mahia ikielezwa amevunja mkataba nao, Gnamien ameifungua mabao mawili aliyowatungua wapinzani wa jadi wa Gor, AFC Leopards katika pambano la ‘Mashemeji Derby’.


Bao moja alifunga kwa kichwa na jingine la shuti la mguu wa kulia kuthibitisha kuwa, anafunga vyovyote akiwa ndani ya eneo la adui.


Inaelezwa straika huyo ameikacha Gor kutokana na kukabiliwa na hali mbaya ya kifedha hasa tangu waliokuwa wadhamini wao na wale wa Ligi Kuu kujiondoa Kenya, hivyo kwa ofa aliyowekewa mezani na mabosi wa Yanga akaona asipishane na mfuko wa fedha na kutua Jangwani.




NIYONZIMA, NCHIMBI FRESHI


Juzi Alhamisi asubuhi Hersi Said alimaliza kazi pale Uganda akimsainisha mshambuliaji Ditram Nchimbi na kumalizana naye kila kitu akichukua mkataba wa miaka miwili kisha akachukua pipa hadi Kigali, Rwanda na usiku huohuo akamaliza kazi nyingine katika Hoteli ya Marriot akimsainisha kiungo wao wa zamani Haruna Niyonzima ambaye alisaini mkataba wa miaka miwili.


Niyonzima tayari alishamaliza mkataba wake wa miezi sita na AS Kigali ambapo Yanga inahitaji kiungo mwenye ubora wa kujua kupiga pasi za mwisho na kuchezesha timu.




AUSSEMS ACHEKA JEURI YA YANGA


Yanga jana Ijumaa waliipa ugumu Simba uvumi ukienea kwamba aliyekuwa kocha wa wekundu hao Patrick Aussems yuko njiani kutua Jangwani, mwenyewe aliposikia akachekaaa alafu akasema uvumi tu tulieni wala siji.


Aussems kwa sasa bado yuko kwao Ufaransa akila maisha baada ya Simba kumsitishia mkataba ambapo alisema hakuna ukweli halisi kwamba atakuja kuwa kocha wa Yanga.

Post a Comment

0 Comments